14 Julai 2025 - 00:46
Uharibifu wa rada ya Kijeshi ya Marekani huko Qatar baada ya Kushambuliwa na Makombora ya Iran

Ulinzi wa anga wa kituo cha Marekani ulifeli Kuzuia Makombora ya Iran, na ajabu ni kwamba Iran ilichagua kuitwanga Kambi hiyo kwa kutumia Makombora ya Zamani.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Iran iliyatwanga maeneo muhimu ya Kambi ya Kijeshi ya Marekani ya Al-Udaida iliyopo Nchini Qatar.  Kuna nukta 4 za msingi kuzifahamu katika shambulizi la Iran dhidi ya Kambi hiyo. Nukta hizo 4 ni kama ifuatavyo:

1️⃣ Matumizi ya Makombora ya zamani aina ya "Qadr H"
Katika shambulio hili. Iran ilitumia Makombora ya masafa marefu ya kizazi cha zamani, yanayojulikana kama Qadr H. Hili linaonyesha kuwa hata teknolojia ya zamani bado ina uwezo wa kufanya mashambulizi sahihi na kugonga Shabaha zake bila kizuizi chochote.

2️⃣ Makombora yalirushwa kutoka umbali mrefu:
Makombora ya Iran yalifyatuliwa kutoka katikati mwa Iran, ambapo kuna umbali mkubwa (masafa marefu) kutoka Qatar, jambo linalodhihirisha uwezo wa kimkakati wa Makombora ya Iran kufikia malengo ya mbali.

3️⃣ Usahihi wa kushangaza licha ya teknolojia ya zamani:
Picha za shambulio hilo zinaonyesha kiwango cha juu cha usahihi wa Makombora hayo, kiasi kwamba hakuna haja ya maelezo ya ziada - matokeo yanaeleza yote.

4️⃣ Ulinzi wa anga wa kituo cha Marekani ulifeli:
Licha ya kuwa na muda wa kutosha kugundua na kujibu shambulio hilo, mifumo ya kujihami ya Marekani katika kambi hiyo ilishindwa kabisa, jambo linaloonyesha uwezekano wa uzembe, au mshangao na kupigwa bunbuwazi, au udhaifu katika ulinzi wao. Na hakuna Shaka kuwa udhaifu katika Ulinzi wao ndio ihtimali yenye nguvu kwamba hilo ndio lililopelekea matumizi ya Makombora ya zamani ya Iran kuwa Makali zaidi kwa Kambi hiyo ya Marekani.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha